TIMU MBILI ZA TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA MCHEZO WA PUNJAB NCHINI INDIA
Na John Luhende
Mwambawahabari
Tanzania inatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kombe la Dunia la Kabadi ambalo linataraji kuanza taraehe tatu hadi tarehe 17 mwezi wa 11 mwaka huu nchini India kataika jimbo la Punjab.
“Tunaamini kushiriki kwa timu za Tanzania katika kombe la Dunia la Kabaddi haitosaidia kukua tu kwa mchezo wa kabaddi, ila pia uelewano na ushirikiano kati ya watu wa mataifa haya mawili” alisema Balozi Sandeep Arya.
Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amesema kuwa Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la Punjab na mikoa mingine ya India na kombe hilo litafanyika katika sehemu tofauti zipatazo 14 kwenye jimbo hilo.
Ameongeza kuwa kwaupande wao wana furaha kubwa hasa mara baada ya Tanzania kupata nafasi ya kushiriki katika sehemu zote mbili,timu ya wanawake na timu ya wanaume.
Naye kaimu katibu mkuu wa baraza la michezo la Taifa BMT,Mohamed Kiganja amewashukuru waandaaji wa kombe hilo kwa kuipatia fursa Tanzania kushiriki kwenye kombe hilo kwani huenda ikawa chachu ya kupata mafanikio kupitia mchezo huo kwani mara nyingi huwa Tanzania maranyingi imekuwa ikishindwakupata mafaniko makubwa katika michezo mingine.
Post a Comment