Ads

MATUKIO MUHIMU TRL KATIKA PICHA KWA MWAKA 2016 - 5


UZINDUZI WA BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA TRL ULIOFANYWA NA WAZIRI WA UJENZI , UCHUKUZI NA MAWASILIANO PROFESA MAKAME MNYAA MBARAWA NOVEMBA 16, 2016
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya TRL Makao Makuu ya TRL Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akimkabidhi mkoba wenye vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya TRL Profesa John  Wajanga Kondoro ikiwa ishara ya kuizindua Bodi hiyo mpya ya TRL.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akimkabidhi Nd Martha Maeda Mjumbe wa Bodi mkoba wenye  vitendea kazi .

Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akimkabidhi Mzee Linford Mboma mkoba wenye vitendea kazi kwa niaba ya Waziri siku ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya TRL.

Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akisoma taarifa fupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya TRL siku ya uzinduzi wa Bodi hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza kwa niaba ya Wajumbe Bodi kabla ya  kumkaribisha  aliyekuwa Msajili wa Hazina Nd Lawrence Mafuru kuzungumza  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo.

Aliyekuwa Msajili wa Hazina Nd Lawrence Mafuru akizungumza  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi  mpya ya TRL kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kuizindua rasmi Bodi hiyo
Novemba 16, 2016

No comments