MATUKIO MUHIMU TRL KATIKA PICHA KWA MWAKA 2016-4
UZINDUZI WA HUDUMA MPYA YA TRENI YA JIJI KWENDA PUGU ULIOFANYWA NA WAZIRI PROFESA MAKAME MNYAA MBARAWA AGOSTI 9, 2016
Treni ya Pugu kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam ikiwa tayari kuzinduliwa na Mgeni rasmi AGOSTI 09, 2016 |
Mageni Rasmi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akihutubia wakati wa hafla ya kuzindua huduma ya usafiri wa Jiji kwenda Pugu , kabla ya uzinduzi rasmi! |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Nd Paul Makonda akitoa nasaha zake kabla ya mgeni rasmi hajazindua treni ya Pugu! |
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Nd Isaya Mwita Charles akitoa nasaha zake kabla ya mgeni rasmi hajazindua treni ya Pugu! |
Wanareli na Wasafiri wakisikiliza nasaha za viongozi wa kitaifa kabla ya uzinduzi wa treni ya Pugu! |
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja kadogosa akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa treni ya Pugu. |
Mgeni Rasmi Profesa Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akipungia bendera ya kijani ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi huduma ya treni ya Jiji kwenda Pugu Agosti 09, 2016. |
Post a Comment