MATUKIO MUHIMU YA TRL KATIKA PICHA 2016 ! - 1
UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA TRL
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Februari 2, 2016 alitangaza uteuzi wa Nd Masanja Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye alikuwa anakaimu nafasi hiyo kuanza likizo ya kustaafu. Uteuzi huo ulianza mara moja.
Kabla ya Uteuzi huo Nd Kadogosa alikuwa Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB)
Nd. Masanja Kungu Kadogosa Mkurugenzi Mtendaji TRL |
Aidha mnamo Julai 01, 2016, Nd Kadogosa alithibitishwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji kamili wa TRL.
MARA TU BAADA YA UTEUZI ALIANZA KAMPENI DHIDI YA UBADHIRIFU NDANI NA NJE YA TRL NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Nd. Masanja Kadogosa Mtendaji Mkuu wa TRL akifanya kampeni Buguruni kwa Mnyamani na Tabata Mwananchi dhidi ya wizi wa kokoto katika njia ya reli ya Dar hadi Ubungo Maziwa mwezi Juni, 2016
Nd. Masanja Kadogosa Mtendaji Mkuu wa TRL akizungumza na Wanareli mara baada ya zoezi la usafi ambalo hufanyika kila siku ya Jumamosi inayoangukia juma la mwisho la mwezi. |
Nd. Masanja Kadogosa Mtendaji Mkuu wa TRL akizungumza na Wanareli mara baada ya zoezi la usafi ambalo hufanyika kila siku ya Jumamosi inayoangukia juma la mwisho la mwezi. |
Post a Comment