SALAAM ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL
SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL
ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA
Nd Masanja Kadogosa |
Ndugu Wanareli Wenzangu;
Nawatakia Mwaka mpya 2017 mwema, kama nilivyotangulia kusema awali, Naamini 2017 utakuwa wa mafanikio makubwa kwenye sekta ndogo hii ya Reli, kila mmoja wetu atimize wajibu hapo alipo, kabla ya kunyoshea kidole mwenzako, jiulize kwanza uwepo wako na unachokifanya kinaharakisha kuyafikia yale
Wanarelii wote tumedhamiria. Tumefanya mengi 2016, tunakila sababu ya kujipongeza na kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi Rehema. Hata hivyo ni vyema tukafahamu adui wa kwanza katika uongozi ni yale mafanikio ya mwisho, ni rahisi uongozi kujisahau na kuzani kila jambo linaenda vyema, mwaka 2017 tutazikabili changamoto zetu kwa nguvu zote, dhamira ya uongozi ni kuona wafanyakazi wetu wanaishi kama wafanyakazi wengine kwenye taasisi za serikali. Kwa pamoja haya yote yanawezekana.
Wasalaam ,
MASANJA KUNGU KADOGOSA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL
Post a Comment