TRENI YA USIKU KWENDA PUGU KUANZA TENA LEO JANUARI 25, 2017!
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
SAFARI
YA TATU AWAMU YA JIONI KWA TRENI YA PUGU KUANZATENA LEO
JANUARI 25, 2017
JANUARI 25, 2017
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
unayo furaha kuwatangazia umma wa Tanzania na Wasafiri wetu wa treni ya mjini (commuter train) iendayo Pugu kuwa safari ya tatu awamu ya jioni itaanza
tena leo siku ya Jumatano Januari 25,
2017. Safari hiyo huanza Kituo kikuu cha
Dar es Salaam saa 2:15 usiku na kuwasili Pugu saa 3:10.
Kuanza tena kwa safari hiyo kunatokana na
kukamilika kwa kazi ya kutandika reli mpya katika eneo korofi kati ya vituo
vya Ilala Block Post na Karakata.
Hata hivyo kwa awamu ya asubuhi safari
zitaendelea kuwa mbili tu kwa vile kazi ya utandikaji reli bado haujakamilika
.Kazi ya ukarabati wa njia ya reli kati ya vituo vya Dar es Salaam na Pugu
ulianza rasmi hapo Januari 02,
2017.
Kazi ya ukarabati huanza kati ya saa 3:15 (09:15 hrs) asubuhi hadi saa 8:15 (14:15 hrs) mchana kila siku
za kazi na inatarajiwa kukamilika
baada ya majuma ( wiki) 10 na tayari majuma ( wiki ) 4 yamekamilika tokea ianze kazi
hiyo.
Ukarabati huu una lengo la kuimarisha njia ya
reli katika eneo hii ambalo kwa sasa linapitisha treni nyingi sana kwa siku
kuliko ilivyokuwa imezoeleka.
Aidha,
ukarabati huu utaondoa kero ya vumbi kwa abiria kwenye mabehewa kwani njia yote itawekewa kokoto za kutosha (stone ballast) ambazo
hazina vumbi.
Ukarabati huu ni wa kubadilisha reli ndogo za
ratili 60 na kuweka reli kubwa za ratili 80 ambazo ni imara zaidi na
kuwezesha kutembea kwa usalama zaidi.
Imetolewa na Afisi
ya Uhusiano kwa Niaba ya:
Mkurugenzi Mtendaji
wa TRL,
Ndg. Masanja Kungu
Kadogosa,
Dar es Salaam
Januari 25, 2017
Post a Comment