WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA MIUNDOMBINU YA BUNGE WAKAGUA HUDUMA YA TRENI YA PUGU!
Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge Mhe Moshi Selemani Kakoso(Mpanda Vijijini) aliongoza Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati hiyo kukagua huduma ya usafiri wa treni ya jiji kutoka Dar es Salaam kwenda Pugu iliyozinduliwa mwaka jana Agosti 29, 2016 na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.
Kabla ya kusafiri na treni hiyo Wajumbe hao walipata taarifa kuhusu chimbuko la mradi huo wa huduma ya treni ya Pugu iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa.
Halikadhalika katika ziara hiyo walikuwepo Maafisa Waandamizi wa Wizara ya kisekta akiwemo Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Edwin Ngonyani , Katibu Mkuu Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho na Mwenyekiti wa Bodi wa TRL Profesa John Wajanga Kondoro.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge wakikagua eneo la ujenzi wa reli ya kisasa 'SGR' pembezoni mwa kituo cha reli cha Pugu leo Machi , 24, 2017 |
Mkurgenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akiwasilisha taarifa fupi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge Makao Makuu ya TRL leo Machi , 24, 2017. |
Aidha ulipowasili ujumbn huo katika kituo cha treni cha Pugu ulipata fursa pia ya kujionea eneo maalum linalo tayarishwa kwa aijli ya uzinduzi wa ujenzi wa reli mpya ya kisasa 'standard gauge railway' (SGR). Mradi huo wenye thamani kubwa unatarajiwa kuzinduliwa kwa kuwekwa jiwe lamsingi hivi karibuni na Raisi wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Magufuli.
Post a Comment