WANARELI WATAKIWA KUBADILISHA MTINDO WA KUFANYA KAZI
WANARELI WATAKIWA KUBADILISHA MTINDO WAO WA KUFANYA KAZI
Mwenyekiti wa Bodi wa TRL Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza na Wanareli wa Morogoro( hawako pichani) |
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akziungumza na Wanareli wa Morogoro (Hawako pichani) |
Bi Mariam Mwanilwa (kushoto) na Bi Martha Maeda Wajumbe wa Bodi ya TRL wakifuatilia kwa makini majadiliano kati ya Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Kondoro na Wanareli wa Morogoro ( Hawako Pichani) |
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Kondoro wakijadiliana kitu na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa m ara b aada ya kuwasili katika Kituo kikuu cha Reli cha dar es Salaam Machi 05, 2017. |
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kuacha kufanya kazi kwa mazoeya na badala yake wajiongeze ili kukabiliana na changamoto za ushindani katika biashara ya usafirishaji nchini.
Ujumbe huu amekuwa akiutoa wakati wa mazungumzo yake na Wanareli wa Tabora, Dodoma na Morogoro katika ziara ya kujitambulisha ya Bodi ya TRL ilioanza Machi 01 Tabora na kumalizika Machi 05, 2017 Dar es Salaam..
Wito huo .Mwenyekiti wa Bodi alikuwa anautoa kila baada kusikiliza michango ya mawazo ya wanareli na kero zao kikazi na kimaslahi..
Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza na Wanareli wa Dodoma hivi karibuni |
Amesema kuwa Bodi ni kiungo baina ya Wafanyakazi, Menejimenti na mwenye mali ambayo ni Serikali. Alitoa wwito kwa Wanareli kuendelea kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na pia kuitaka Menejimenti ikiongozwa na Nd Masanja Kadogosa kuendelea kutatua kero za Wanareli zile zilizo ndani ya uwezo wake.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Nd Kaodogosa amebainisha kuwa Uongozi wa TRL tayari imeshalipa jumla ya Shilingi bilioni 7.1 katika ya Julai , 2016 hadi Februari , 2017. Malipo yalihusu michango katika hifadhi za jamii ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Pia ilidhihirika katika malimbikizo ya nyongeza ya mshahara nyongeza 3 zimeshalipwa katika 5 na hivyo kubakia na nyongeza 2.
Baadhi ya kero zilizoainishwa .katika ziara hiyo ya Bodi ambayo ilihusu kujua matatizo ya miundombinu na kero za Wanareli ni pamoja na kero za maji magengeni, Wanareli kuwepo katika ngazi ya moja ya Utumishi zaidi ya miaka kati ya 10 hadi 20.
Profesa Kondioro aliwaahidi Wanareli wa mikoani kero zao zitakuwa ajenda muhimu katika vikao vijavyo vya Bodi na kusisitiza kuwa wawe wabunifu na kuhimizana kuchapa kazi kwa bidii na kutowavumilia wenzao wachache wanaoshiriki katika vitendo vya hujuma.
Mwanareli wa Dodoma akitoa mchango wake wakati wa klikao na Mwenyekiti wa Bodi Machi 03, 2017 |
Post a Comment