Ads

'BLOCK TRAIN' YA SHEHENA ZA WFP YAZINDULIWA LEO !




Mkurugenzi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford akitoa ruhusa kwa dereva kuanza safari maarufu kama 'line clear'.



Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Kondoro akipunga bendera 'flag off' kuruhusu tgreni kuanza mendo kuelekea Dodoma na shehena ya mahindi tani 800.















Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Wajanga Kondoro leo Aprili 24, 2017, amezindua huduma ya treni ya moja kwa moja 'block train' kwa ajili ya shehena za mahindi ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenda katika ghala yao kuu mjini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa TRL Nd. Masanja Kadogosa akitoa taarifa kuhusu huduma ya 'block train' ya WFP.
Katika hafla hiyo iliyofanyika asubuhi katika kituo cha treni cha Malindi bandarini Dar es Salaam imedhihirika kuwa WFP imeamua kuanza tena kutumia huduma za TRL baada kuona taasisi hiyo imeimarika kulingamnisha na miaka 3 iliyopita.

Akitoa taarifa fupi ya ufafanuzi Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja  Kadogosa alisema usafirishaji wa shehena kutumia 'block train' una lengo la kutimiza matakwa ya mtyeja ya kufikishiwa mzigo wake kwa haraka na kukidhi mahitaji ya walaji.

Alisema WFP waliacha kutumia huduma za TRL baada ya uwezo wake kutetereka hata hivyo baada ya kuiimarika na kujipanga vyema kiutendaji TRL iko tayari kukabiliana na changamoto ya kuhudumia shehena ya WFP.
" Shehena ya tani 7000 zza mahindi tunamuhakikishia Mkurugenzi wa WFP tutaikabili kama ipasavyo na kuisafirisha ndani ya siku 10 tulizokubaliana na WFP'. Alisisitiza Ndugu Kaodogosa.
Hata Mtebndahji huyo qwa TRL alitoa abngalizo kuwa kwa TRA na TPA kuwa urasimu wa kutoa kibali vya kuruhusu mizigo uharakiushwe kama inavyofanyika kwa malori ili TRL iweze kutimiza malengo yake ya  kuusafirisha tani hizo 7000 za mahindi kwa wakati.

Naye Mwakilishi wa WFP nchini Bwana Michael  Dunford alisisitiza kuwa ushirikiano wa taasisi kubwa za WFP na TRL zinadhihirisha maborsho yaliyofanywa na Serikali kwa kuipatia TRL mnyezo mpya vikiwemo vichwa vipya vya treni na mabehewa. Alisisiitiza kuwa WFP imeamua kutumia zaidi bandari ya Dar es Salaam kusafirisha shehena zake za misaada na kwamba njiani kuna meli m,bili zinatarajiwa kuleta shehna kubwa zaidi .

Imefahamika jumla ya 'block train' 9 zitahitajika kusafirisha tani hizo 7000 za mahindi kwenda Dodoma.zitakazoiingizia TRL jumla ya Dola za Kimarekani $217,000/=.
.
Mwakilishi wa Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford akitoa salaam zake wakati wa hafla uzinduzi wa 'block train' ya WFP kwenda  Dodoma iliyofanyika 'Malindi Yard' bandarini Dar es Salaam. 

Mwenyekiti wa Bodi TRL Profesa John Kondoro akiteta na Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa 



Mwenyekiti Profesa John Kondoro akipongezwa baada ya kuzindua 'block train ' ya WFP.






















No comments