Ads

HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KUANZIA TENA DAR JUMAPILI JUNI 11, 2017

Huduma ya usafiri wa Abiria kuanza tena Dar siku ya Jumapili Juni 11, 2017. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Focus Makoye Sahani amewaeleza Waandishi wa habari jana asubuhi makao makuu ya TRL Dar es Salaam. Amesema kuwa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo zilihamishiwa kwa muda mjini Morogoro kuanzia Mei 20, mwaka huu baada ya daraja mojawapo katika mto ruvu kutitia. Kazi ya ukarabati wa daraja hilo ilikamilika Juni 2, 2017. Hadi wakati huu inapoamriwa kuwa treni za abiria nazo zianzie Dar takriban treni za mizigo 15 zimeshapita katika daraja hilo bila ya mushkeli wowote.. Habari zaidi ni katika picha ikiwemo za ukaguzi wa daraja uliofanyika juzi Juni 07, 2017.










No comments