Leo mchana Septemba 29, 2017, Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Nchini (Rahco) imeingia mkataba na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki kujenga kipande cha pili cha reli ya kisasa ya Standard gauge(SGR) kutoka Morogoro hadi Makutopora chenye umbali wa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishana treni na maeneo ya kupangia mabehewa jumla kilomita 422 kwa uzani wa tani 35 kwa ekseli.
Kandarasi hii itakuwa na thamani ya jumla TZS Trilioni 4.3, mkataba umetiwa saini na Mtendaji Mkuu wa Rahco na TRL Nd Masanja Kadogosa na Mwanasheria wake Nd Petro Mnyeshi na kwa upande wa Yapi Merkezi waliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi wake Bwana Erdem Ariogl na Mkuu wa Miradi ya Ethiopia na Tanzania Bwana Abdullah Alli .
Wakati huohuo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema utiaji sahihi wa kandarasi hii ya pili ni kuonesha dhamira isotetereka ya Serikali ya awamu ya 5 kuendeleza na kuimarisha miundo mbinu ya reli nchini kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya kiuchumi nchini.Amesema reli ya kisasa ya SGR italeta mabadiliko makubwa sana kiuchumi na kijamii na maendeleo kwa jumla. Kwanza zitaokoa uharibifu wa barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa. Bidhaa zinazosafirishwa kwa masafa marefu zitafika kwa gharama ndogo hivyo walaji watazinunua kwa bei nafuu.
Hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Ruaha katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(JKNICC) ilihudhuriwa na kaimu balozi wa Uturuki nchini pamoja na Wawakiishi wa Kampuni ya Yapi Markezi. Wengine waliohudhuria ni Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano wakiongozwa na Katibu Mkuu wa WUUM -Uchukuzi Mhandisi Dk Leonard Chamuriho.
Mapema mwaka huu Februari 03, 2017, Yapi Merkezi na Mota Engil ya Ureno ziliingia mkataba na Rahco wa kujenga kipande cha kwanza cha reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro urefu wa jumla wa Kilomita 303. Ujenzi wa kipande hicho ulitiwa jiwe la msingi na Rais wa Tanzania Dk John Magufuli hapo Aprili 12, 2017 katika hafla kubwa ya aina yake iliyofanyika katika kituo cha Reli cha Pugu nje ya jiji la Dar es salaam.
Habari zaidi katika picha.........
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge Nd Hawa Ghasia akibadilishana mawazo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, wakati Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano akipitia baadhi ya nyaraka za mkataba SGr-2 Moro-Makutopora katika hafla ya utiaji saini JKNICC Dar es Salaam, Septemba 29, 2017.
|
|
Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi ya Mkandarasi Yapi Merkezi Bw Erdem Ariogl akitoa neno kwa niaba ya Uongozi wa juu wa Yapi Merkezi siku ya ujtiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora ndani ya ukumbi wa Ruaha katika kituo cha JKNICC, jijini Dar es Salaam, Septemba 29, 2017.
|
|
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano(WUUM) akihutubia hadhara kabla ya utiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora hafla iliyofanyika JKNICC jijini Dar es Salaam, siku ya Ijumaa Septemba 29, 2017.
|
|
Wawakilishi kutoka Mkandarasi Yapi Markezi ya Uturuki
|
|
Mkataba umetiwa saini na Mtendaji Mkuu wa Rahco na TRL Nd Masanja Kadogosa na Mwanasheria wake Nd Petro Mnyeshi na kwa upande wa Yapi Merkezi waliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi wake Bwana Erdem Ariogl na Mkuu wa Miradi iliopo Ethiopia na Tanzania Bwana Abdullah Alli.
|
|
Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi ya Yapi Merkezi Bwana Erdem Ariogl akibadilishana hati za Mkataba na Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Nd Masanja Kdogosa.
|
|
Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi ya Yapi Merkezi Bwana Erdem Ariogl na Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Nd Masanja Kdogosa wakionesha nakala za mkataba wa SGR-2, Moro-Makutopora mara baada ya kusainiwa JKNICC jijini Dar es Salaam , Septemba 29, 2017.
|
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akiwapongeza Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Bodi ya Yapi Merkezi Bwana Erdem Ariogl na Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Nd Masanja Kdogosa baada ya kukamilika zoezi ya utijai saini mkataba wa SGr-2, Moro-Makutopora.
|
|
Picha ya ukumbusho
|
|
Katibu Mkuu WUUM-Uchukuzi Mhandisi Dk Leopnard Chamuriho akipokewa na Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Nd Masanja Kdogosa alipowasili JKNICC kushuhudia kusainiwa SGR-2 , Septemba 29, 2017.
|
|
Katibu Mkuu-WUUM Mhandisi Dk Leonard Chamuriho kwa pamoja na Wahandisi Ujenzi wa Rahco Maizo Mgedzi na Felix Nnaliho wakipitia nyaraka za mkataba wa SGR-2, Morogoro-Makutopora, JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Pichani Wakurugenzi wa Bodi ya TRL Mzee Linford Mboma( wa kwanza kulia mstari wa mbele) na Mhandisi Charles Mvungi walihudhuria hafla ya kusainiwa mkataba wa SGR-2, Morogoro-Makutopora, JKNICC, Septemba 29, 2017
|
|
Wanareli kutoka TRL na Rahco wakifuatilia hafla ya utiaji saini SGR-2 Moro-Makutopora , JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Katibu Mkuu WUUM Mhandisi Dk Leonard Chamuriho akliwatambulisha wageni mashuhuri katika hafla ya utiaji saini JKNICC Septemba 29, 2017
|
|
Wanareli kutoka TRL na Rahco wakifuatilia hafla ya utiaji saini SGR-2 Moro-Makutopora , JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge Nd Hawa Ghasia akitoa neno kuhus umuhimu wa ujenzi wa reli mpya ya SGR.
|
|
Mtendaji Mkuu wa Rahco na TRL Nd Masanja Kadogosa akitoa taarifa ya mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora, JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Mtendaji Mkuu wa Rahco na TRL Nd Masanja Kadogosa akitoa taarifa ya mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora, JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Mtendaji Mkuu wa Rahco na TRL Nd Masanja Kadogosa akifafanua jambo wakati akitoa taarifa ya mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora, JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Kaimu Balozi wa Uturuki akitoa neno siku ya utiaji saini mkataba wa SGR -2 Moro-Makutopora, Septemba 29, 2017, JKNICC Dar es Salaam.
|
|
|
Kaimu Balozi wa Uturuki akitoa neno siku ya utiaji saini mkataba wa SGR -2 Moro-Makutopora, Septemba 29, 2017, JKNICC Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mkuu WUUM Mhandisi Dk Leonard Chamurih akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano(WUUM) kuhutubia hadhara kabla ya utiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora hafla iliyofanyika JKNICC jijini Dar es Salaam, siku ya Ijumaa Septemba 29, 2017.
|
|
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano(WUUM) akihutubia hadhara kabla ya utiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora hafla iliyofanyika JKNICC jijini Dar es Salaam, siku ya Ijumaa Septemba 29, 2017.
|
|
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano(WUUM) akihutubia hadhara kabla ya utiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora hafla iliyofanyika JKNICC jijini Dar es Salaam, siku ya Ijumaa Septemba 29, 2017.
|
|
Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Masanja Kadogosa akisalimiana Nd Midladjy Maez mmiliki wa Maez Blog na Mwanareli wa siku nyingi mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa SGR 2 kukamilika.
|
|
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano(WUUM) akisalimiana Nd Midladjy Maez mmiliki wa Maez Habari Blog na Mwanareli wa siku nyingi mara baada ya kukamilika kwa hafla ya utiaji saini Mktaba wa SGR-2 , JKNICC, Septemba 29, 2017.
|
|
Mtendaji Mkuu wa TRL na Rahco Masanja Kadogosa akimkaribisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa -WUUM mara baada ya kuwasili katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JKNICC Dar es Salaam tayari kwa utiaji saini mkataba wa SGR-2 Moro-Makutopora. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu WUUM Mhandisi Dk Leonard Chamuriho.
|
Post a Comment