RAIS MAGUFULI KUKIPAISHA KISWAHILI KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE !
Punde tu nimechapisha tena Makala yenye takriban umri wa miaka 10 kuhusu umuhimu wa KUKIPA HADHI NA DHIMA INAYOSTAHILI LUGHA YETU YA KISWAHILI KATIKA MIKAKATI NA MIPANGO YA KUHARAKISHA MAENDELEO NCHINI NA HASA KUTUMIKA KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU!
Napenda kuchukua fursa hii kutambua mchango mkubwa wa Rais wetu Dk John Magufuli kwa kukipa hadhi ya pekee kiswahili hususan wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wageni wake Wakuu wa nchi Ikulu Dar es Salaam. Hili jambo halijawahi kutokea katika awamu zote nne zilizopita!
Baada ya Mkuu wa nchi kuonesha njia sasa wote waliokuwa katika nyadhifa mbali mbali za kidola wachukulie huo uamuzi wa Rais kuwa ni amri na waanze kuweka mikakati ya muda mfupi, kati na mrefu ili sasa tuwe na shida moja tu kupata wakalimani wa kimataifa wa kutosha.
Ni aibu nchi za Kenya, Rwanda, Malawi, Uganda, Burundi na DRC kutambuliwa kutoa Wataalamu wa Kiswashili wakati sisi Watanzania tupo tunazubaa zubaa tu.
Kule Umoja wa Afrika Addis (AU) wanataka Wataalamu wa lugha hii ya Kiswahili . Mathalan wakati wa awamu ya 4 Rais Ali Bongo wa Gabon aliomba apelekewe Mwalimu wa Kiswahili sijui kama ombi lake lilitekelezwa?
Shime wakati haumngojei mtu JPM ameonesha njia tusitembee bali tukimbie. Rais ametoa changamoto kwa taasisi zote zenye dhima ya kukuza lugha hii adhimu ya kiswahili! HATIMAYE MKOMBOZI WA LUGHA YA KISWAHILI KUKIREJESHEA HADHI YAKE NA KUKIPA DHIMA YAKE KUONGOZA MAPINDUZI NA MAENDELEO YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA AMEPATIKANA NI NDUGU RAIS DK JOHN MAGUFULI! HONGERA SANA MHESHIMIWA RAIS!
Post a Comment