Rais wa Tanzania Dk John Magufuli leo Septemba 10, 2017 amemteua rasmi Profesa Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman .
Kabla ya uteuzi wa leo Profesa Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo ya Jaji Mkuu.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imefafanua kuwa Jaji Mkuu mpya ataapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam, kesho Septemba 11, 2017, saa 4 asubuhi.
|
Mhe Profesa Ibrahim Juma Jaji Mkuu Mteule wa Tanzania |
|
Rais John Magufuli hapo Januari 17, 2017 akimpongeza Profesa Ibrahim Juma alipomuapisha kuwa Kaimu Jaji Mkuu Ikulu Dar es Salaam |
|
Picha kama hii kesho itajirudia Ikulu lakini itakuwa katika hadhi tofauti ambapo Profesa Ibrahim Juma atakuwa ameapishwa rasmi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania leo ni Jaji Mkuu Mteule! Hongera Profesa! |
.
Post a Comment