Ads

NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA TRL KUFAHAMU CHANGAMOTO ZAKE!

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye aendelea na ziara ya kujitambulisha katika Taasisi zilizo chini ya Sekta anayoliongoza leo Jumatano Oktoba 25, 2017 alipiga hodi Makao Makuu ya Kampuni ya Reli (TRL) jiini Dar es Salaam na kupokelewa na Mtendaji Mkuu Nd Masanja Kadogosa ambaye alimwongoza hadi chumba cha mkutano. Katika chumba cha Mkutano Mtendaji Mkuu wa TRL alitambulisha Maafisa waandamizi wa TRL waliokuwepo ukumbini.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji Nd Focus Makoye Sahani alitoa taarifa ya uendeshaji wa huduma za reli ikiwemo ya jijini Dar na zile za abiria kwenda Bara na pia usafirishaji  shehena kwenda bara na nchi jirani. Waandishi wa Habari ambao walikuwa wamefurika katika ziara hiyo, baadhi ya maswali yao yalihusu zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo ya njia ya reli. Naibu Waziri aliungana na Mtendaji Mkuu wa TRL kwa kupigilia msumari kwa kusema kuwa maeneo ya reli yaliovamiwa ni ya Serikali na kwamba kama mwananchi ameendeleza maeneo hayo ambayo sio halali, sheria imetamka wazi kuwa kutojua sheria sio utetezi wa mhusika kutoadhibiwa. Hivyo ametoa wito kwa wananchi kuwacha wazi maeneo yalioainishwa kisheria kuwa ni ya reli na barabara ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima endapo mtu atasubiri hadi  akumbwe na zoezi la bomoabomoa!........Habari zaidi katika picha!

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipokewa na Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa.

Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa. akimkaribisha Naibu Waziri -MU

Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa. akimkaribisha Naibu Waziri -MU

Pichani baadhi ya Maafisa Waandamizi wa TRL na Rahco

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji Nd Focus Makoye Sahani alitoa taarifa ya uendeshaji wa huduma za reli kwa Naibu Waziri -MU

Pichani Waandishi wa Habari wakiwajibika.

Pichani baadhi ya Maafisa Waandamizi wa TRL 

Pichani baadhi ya Maafisa Waandamizi wa TRL na Rahco

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye

Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa. akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo!


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari.

Pichani Waandishi wa Habari wakiwajibika.

No comments