Ads

WALIOGAWA MAENEO YA HIFADHI YA RELI KUSHUGHULIKIWA NA SERIKALI!

WALIOGAWA MAENEO YA HIFADHI YA RELI KUSHUGHULIKIWA NA SERIKALI!


SERIKALI  imesema inawafuatilia  baadhi ya viongozi  waliotumia madaraka  yao vibaya kwa  kuwapatia wananchi  maeneo ya hifadhi za reli  huku wakijua ni kinyume cha sheria.
Pia  imetenga  TZS.bilioni 14 kwa ajili ya kurudisha  njia ya  reli  ya Arusha hadi  Moshi kutokana na eneo hilo  kuonekana kuwepo  na wafanyabiashara  wengi.
Tamko hilo  lilitolewa na  Naibu Waziri wa Uchukuzi kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye  jijini Dar es Salaam jana, wakati alipofanya ziara  ya  kutembelea Kampuni ya Reli  nchini (TRL) kwa lengo  la  kujitambulisha  tokea   baada ya kuteuliwa na Rais  Dk. John  Magufuli  katika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano akisimamia sekta za Uchukuzi na Mawasiliano.

Alisema  viongozi hao  ni  lazima wafuatiliwe kwani   wamekuwa sababu ya kuwepo   kwa  changamoto nyingi  katika taasisi ya  usafiri wa reli nchini.
Mhandisi  Nditiye alisema   changamoto hizo zimetokana na baadhi ya  wajanya  kushirikiana na   wananchi kuweza kuvamia maeneo ya reli huku  wakitambua kuwa ni kinyume cha sheria.
“Kwa wafanyakazi waliofanya hivyo ni lazima tuwafuatilie kwani lazima  tujenge  utamaduni  kwa  wananchi wa  kuweza  kuheshimu  mali za serikali,”  alisema.
Pia  kutokana  na hilo, Mhandisi   Nditiye aliwataka wananchi wote waliojenga  eneo lolote  la hifadhi  ya reli  kubomoa  mara moja ili kupisha  mradi wa  ujenzi na uboreshaji wa  reli  nchini.
Alifafanua kwa wananchi ambao  mradi wa  reli umegusa maeneo yao , Serikali  imeiomba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi kufanya tathimini  kwa ajili ya kuwalipa.
Kwa upande mwingine, Mhandisi  Nditiye, aliwaasa  wafanyakazi wa TRL  kuhakikisha   wanafanya kazi kwa kusimamia  mpango wa maendeleo  na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“ Haitapendeza  kuona mtu  anaenda kinyume  na azma  ya serikali  katika utekelezaji  wa majukumu kwani  hatua  kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.
Kwa upande mwingine  serikali imetenga  TZS. bilioni 14 kwa ajili ya  kurudisha  njia ya  reli  ya Arusha hadi  Moshi kutokana na eneo hilo kuwepo  na wafanyabiashara  wengi.
Akitolea ufafanuzi  suala hilo, Mkurugenzi  Mtendaji wa TRL, Nd. Masanja  Kadogosa  alisema  njia hiyo inatarajiwa kuwa tayari kutumika ifikapo Julai  mwaka 2018 ambapo kiasi cha  fedha kilichotengwa kitasaidia kukarabati   madaraja  na vituo  vya  reli.
“ Tunafanya hivyo kwa  eneo  Arusha hadi Moshi kwani   limeonekana  kuwa   na biashara  nyingi, hivyo tunawaomba wananchi wakae mkao wa kula ili kuwezesha serikali  kupata mapato yanayostahili kupitia sekta ya usafiri wa reli,”alisema.
Hata hivyo alizitaja  baadhi  ya changamoto wanazokabiliwa nazo kuwa ni jinsi ya  upatikanaji wa vibali  vya wafanyakazi wa kigeni, Vitendea kazi  na  Ubovu  wa mtandao wa reli ya kati ambao umechakaa kwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100.



Naibu Waziri wa Uchukuzi kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye  akizungumza na Waandishi wa Habari hapo jana.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji wa TRL Nd Focus Sahani akitoa taarifa ya uendeshaji wa TRL kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsiliano ( Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano) , Mhandisi Atashasta  Nditiye hapo jana.  

Pichani Waandishi wa habari wakiwa kazini.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsiliano ( Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano) , Mhandisi Atashasta  Nditiye hapo jana. akizungumza na Waandishi wa habari.

 Mtendaji Mkuu wa TRL  Nd Masanja Kadogosa.akifafanua jambo wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsiliano ( Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano) , Mhandisi Atashasta  Nditiye Makao Makuu ya TRL jana jijini Dar es Salaam.


No comments