Nawatakia Siku Kuu njema ya Krismas Wanazengo!
Usione hivi ...hawa jamaa uhasama wao umeanza dahari na dahari sikiliza hiki kisa cha kitabuni: Mbwa na paka waliombeana mabaya ndani ya Safina! Nabii Nuhu alipiga marufuku viumbe kushughulika ndani ya safina. Mbwa walizidiwa na mahanjam wakaanza kushughulika kabla ya kufikia tamati paka wakawafuma na kushitaki kwa Nabii Nuhu ambaye aliwalaani ndio maana mbwa wanagandana kishenzi mpaka 'mabuja' yote yanywee ndio wanaachana! Sasa wakati viumbe vikiwa ndani ya safina mbingu zilikuwa wazi hivyo kiumbe akiomba kitu kwa Mola alikubaliwa(Fikiria wanaume wenye viba100 wangeomba nini?)!Mbwa nao wakiwa katika hali ya kudhalilika nao wakamuomba Mola kuwa paka nao wakitaka kushughulika basi nao iwe muhadhara kila mtu ajue!😀 Hivyo basi iwe jioni au usiku wa manane watu lazima watajua kuwa paka wanataka kushughulika kutokana na miguno na kelele wanazopiga wakiwa katika mchakato wa kushughulika. Hivyo basi paka wakitaka kushughulika au hata wanaposhughulika mtu lazima atajua! Good Morning I wish you Merry Christmas!🙏🏻🥂🍾💃🕺
Post a Comment