Ads

TANZANIA MBIONI KUPATA CHETI CHA NCHI ZENYE VIGEZO VYA KUDHIBITI RASILIMALI KUTOTUMIKA KUENDELEZA MACHAFUKO

Na Mwandishi Maalum

Imeelezwa kwamba ndani ya Miaka miwili ijayo Tanzania inatarajiwa  kupata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi iliyokidhi Vigezo vya nchi zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini kuepusha machafuko kwa nchi wanachama. 

Cheti hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kuruhusu Madini ya Bati (tin), dhahabu kuuzwa nje ya nchi yakiwa yametambuliwa na kuthaminiwa

 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongoza Sekretarieti iliyofanya tathmini ili kujiridhisha na endapo Tanzania inaweza kupewa cheti ili kuwa miongoni mwa nchi zinazokidhi vigezo kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza makubaliano ya kutokuruhusu rasilimali za nchi kutumika kuchochea maasi wakiendelea na mazungumzo baada ya taarifa ya tathmini kuwasilishwa Juzi usiku tarehe 18 Desemba, 2018 jijini Dar es Salaam 


Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo  juzi tar Desemba 18,  2019 jijini Dar es Salaam,  kilicholenga  kupokea ripoti juu ya tathmini iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa ya kutunza rasilimali za nchi ili zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko kwa nchi wanachama. 

Ripoti hiyo iliwasilishwa na wajumbe kutoka kwa viongozi wa sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu wenye nchi wanachama 12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali zinazopatikana katika nchi zao ili zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko katika nchi wanachama. 

Akizungumza katika kikao hicho,  Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alisema anatarajia nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa pamoja ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho. 

Wajumbe wakiendelea na majadiliano

Nyongo alisema kwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieri wakati ilipokuwa  nchini, imewaonesha wazi namna Serikali ya Tanzania inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.

Akizungumza mchakato huo, Gerard Nayuburundi mmoja Kati ya wajumbe wakiokuwa wakifanya tathmini nchini kutoka Burundi alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho. 

Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili kile  walichowekeza nchini kiwe na matokeo chanya.


No comments