Ads

Watoto wa Ibilisi’ wazua hofu Tanga “wanaua, kukaba, kupora kwa silaha”






Vikundi vya uhalifu vimeibuka Jijini Tanga na kuzua taharuki kwa Wananchi baada ya kundi linalojiita “Watoto wa Ibilisi “, kujeruhi watu zaidi ya kumi na kumuua Mwenyekiti wa Kata ya CentUral kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali pamoja na kupora mali na fedha.

Hoja hiyo imeibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakati wakipokea taarifa za kamati mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2018/2019.

Aidha DC Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wananchi wa Jiji hilo kuwa watulivu kwani Kamati ya Ulinzi na Usalama ipo kazini kuhakikisha inarudisha hali kuwa shwari


No comments