HABARI KATIKA PICHA: TANZANIA YAONGOZA KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKADI KATIKA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA POSTA AFRIKA
Yaya Sangare, Waziri wa Mawasiliano wa Mali (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) Hati ya kuitambua na kuipongeza Tanzania kwa kuongoza katika utekelezaji wa Mpango wa Anuani za Makazi na Postikodi kati ya nchi wanachama 45 wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU). Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya PAPU yaliyofanyika Jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro(wa tatu kulia) katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya PAPU,yaliyofanyika Jijini Arusha.
Post a Comment