Ads

RAMANI YA ENEO LA KIWANJA KWA AJILI YA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA PAPU ARUSHA YAKABIDHIWA RASMI



Na Mwandishi Maalum, Arusha

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano 

Mhandisi Isack Kamwelwe juzi Januari 8 mwaka 2020 amemkabidhi rasmi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mashirika ya Posta Afrika(PAPU).

Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe  Mkandarasi wa jengo hilo ni Kampuni ya Beijing Construction , Liang Li na jengo na litajengwa ndani ya Jiji la Arusha na linakadiriwa kugharimu Sh.bilioni 30 .

Akizungumza wakati wa kukabidhi eneo hilo Mhandisi Kamwelwe amesema  ujenzi huo umekuja muda muafaka kwa kipindi cha Rais wa Awamu ya Tano Dk.John Magufuli ambaye  anafata nyayo za Baba Wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na anaamini kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati

"Kuna nchi 45 Wanachama wa Mashirika ya Posta katika nchi za Afrika 1980 walikaa na kukubaliana Makao Makuu ya PAPU yawe hapa nchini Tanzania na Baba wa Taifa akakubaliana nao na wakapanga yajengwe Arusha na ndio maana katika kuadhimisha miaka 40 ya Mashirika haya tumeamua tuanze kujenga jengo la Makao Makuu ya Mashirika haya ya Posta Afrika" amesema Waziri Kamwele.

Amesema jengo hilo litakuwa na ghorofa 16 na kugharimu TZS 30  na kwamba linatakiwa kujengwa na kumalizika kwa kipindi cha miezi 30 huku akimtaka Mkandarasi wa jengo hilo kujenga katika ubora unaotakiwa na viwango vya Serikali .

Amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wafanyakazi wao ambao wanatoka nje ya nchi kuja na nyaraka zote za uhamiaji pamoja na vibali vya kufanyia kazi hapa nchini.



 Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe  akimuonyesha mkandarasi  ramani ya jengo hilo la Makao Makuu ya Mashirika ya Posta Afrika(PAPU), jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa 16  na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30 (picha na Woinde Shizza,Arusha)



  Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akimuelekeza mkandarasi eneo la uwanja lililopo jiji Arusha kwa ajili ya ujenzi Wa jengo la  Makao Makuu ya Mashirika ya Posta Kwa nchi za Afrika(PAPU), litakalo gharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 30 (picha na Woinde Shizza,Arusha).



 Msimamizi na mshauri wa ujenzi wa jengo hilo  Nathanael Alute  kutoka kampuni ya B.J. Amuli  Architects akitoa maelezo mbele ya Waziri Kamwelwe.


"Jengo hilo ni Makao Makuu ya Mashirika ya Posta Afrika(PAPU), hivyo hairuhusiwi mtu yeyote asiehusika kuingia katika eneo hili bila kibali kutoka kwa wahusika ,eneo hili ni la kimataifa halitakiwi kuingia bila kibali iwapo mtu atakutwa anazubaa humu hatua kali za kisheria,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk Jones Kilembe ameishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoonyesha usimamizi na ufuatiliaji hadi kufikia hatua ya kupatikana eneo rasmi na tayari kwa uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo hilo la Makao Makuu ya PAPU.

Amewataka wananchi wa Arusha kutoa ushirikiano katika masuala ya  ulinzi hata ikitokea katika eneo la uchangiaji huku akiongeza  kuwa watamsimamia vyema mkandarasi huyo na kuhakikisha anamaliza kazi kwa muda uliopagwa na ikiwezekana hata kabla ya muda uliopangwa kufika.

Wakati huo huo Mkuu Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameishukuru Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kujenga Makao Makuu ya PAPU  jijini Arusha.

Ambapo amesema  kwa nafasi yake atashirikiana nao vyema katika kutatua vikwazo vyote vilivyopo ndani ya uwezo wake katika nafasi ya ngazi ya mkoa ili kuhakikisha mkandarasi anamaliza Kazi kwa wakati.

Msimamizi na Mshauri Wa jengo hilo Nathanael Alute kutoka kampuni ya B.J. Amuli Architects amesema kuwa atasimamia vyema ujenzi huo uwe wa viwango vinavyotakiwa na serikali na kumalizika kwa muda uliopangwa huku akijitaidi gharama za ujenzi zisiwe kubwa zaidi.



 Mkandarasi  wa kampuni ya Beijing Construction Enginering Group,  Liang  Li akimueleza Waziri Kamwelwe kuwa watakamilisha ujenzi huo wa jengo la Makao Makuu ya PAPU kwa wakati



Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akiongea na Waziri  Kamwelwe ambapo alimuhaidi kulinda eneo hilo huku akitoa onyo kwa Mtu  yeyote ambae atakutwa katika eneo hilo bila kibali kuchukuliwa hatua Kali za kisheria(picha zote na Woinde Shizza,Arusha).


No comments