Ads

Wasafi wafikiria kumiliki timu ya kandanda nchini!

Rais wa FIFA Gianni Infantino( wa kwanza kushoto), Diamond, Fatoumata Samoura Katibu Mkuu FIFA na Rais wa CAF Ahmad Ahmad wakati wa Sherehe za Tuzo za CAF Cairo Misri hivi karibuni

Utashi wa Wasafi  kumiliki timu ya kandanda nchini umejitokeza wakati wa mahojiano mbashara na Mmiliki wa Wasafi Media Diamond Platnumz katika kipindi  maarufu cha Sports Arena hivi leo Januari 10, 2020.

Sports Arena walimualika Diamond ili kufahamu yaliojiri huko Cairo Misri ambako alikuwa Mwanamuziki pekee aliyetumbuiza katika sherehe za kutunuku  tuzo za CAF za mwaka 2019 ambako nyota wa Liverpool na Senegali Sadio Mane aliibuka kidedea kwa Wachezaji wa kiume.

Diamond akiwa katika mahojiano na jopo la Wasafi Sports Arena

Diamond akisisitiza jambo..

Diamond aliwaeleza watangazaji wa Sports Arena ya Wasafi FM kuwa akiwa Cairo alikutana na Rais wa FIFA Gianni Infantino na viongozi wengine wa CAF aliweza kubadilishana nao mawazo jinsi ya kuendeleza soka barani Afrika na hasa Tanzania.

Kuhusu swali kama anafikiria kumiliki timu ya kandanda alijibu ni kweli na angependelea kumiliki timu iliyo katika nafasi nzuri ya ligi  ambayo mchakato ukikamiliki itaitwa Wasafi Sports Club.

Diamond akifafanua jambo..

Alisisitiza tayari huko siku za nyuma washauri wake walimtahadhirisha kuwa kujiingiza katika umiliki wa Klabu ya Soka kutamsababishia hasara kiuchumi.

Maulid Kitenge aliongoza jopo la Sports Arena katika mahojiano na Platnumz
Aidha wakati wa mahojiano hayo kulitangazwa kuwa kituo cha Wasafi media kimetunukiwa Tuzo maalum na Uongozi wa You Tube Duniani kwa kufikisha wafuasi milioni moja na kuvishinda vituo vya majiji ya Vancouver(Canada), Venice Italia na Las Vegas Marekani.

Wakati huohuo nguli huyo wa muziki kuanzia leo Januari 10, 2020 anaanza ziara rasmi za kimuziki nchini Nigeria ,Ulaya, Madagascari(Bukini) na Visiwa vya Ngazija(Comoros) kwa mialiko rasmi.

( Kwa habari zaidi fuatilia Wasafi Media Live katika You Tube na Wasafi FM)


No comments