MHARIRI DEO MUSHI ANATUKUMBUSHA WAJIBU WETU KWA NGAZI YA KAYA JINSI YA KUPAMBANA NA KORONA!
⛑Hi Friend ! PROTECT YOURSELF AGAINST COVID-19 IT IS LETHAL! ☠ KILA MTANZANIA ACHUKUE TAHADHARI KWA KUFUATA KIKAMILIFU MASHARTI YA KUJIKINGA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA COVID-19 KWANI VINAUA HARAKA SANA!☠⛑
Ndugu zangu mimi ni Deo Mushi. Habari ya leo Jumapili.Nadhani wengi mpo na watoto wenu na wajukuu nyumbani baada ya Shule zote jufungwa kutokana na balaa la corona. Naomba kuuliza maswali yafuatayo: Hivi huko majumbani ni hatua gani mnachukua kuhakikisha watoto ni salama? Jumapili leo wamekwenda kanisani? Kuna utaratibu gani wa kukaa huko kwenye nyumba za ibada? Watoto wanapanda daladala wakati huu wa corona kwenda aidha makanisani/misikitini? Watoto na majirani zao wanacheza pamoja? Dada akitoka sokoni au dukani ananawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni? Je nasi tukitoka kwenye mishughuliko yetu tunanawa mikono kabla ya kuingia ndani ya nyumba zetu? Je tuna utaratibu wowote wa kuwapokea wageni wanaotutembelea katika nyumba zetu? Je viongozi wetu tuliowachagua hivi karibuni wanafanya lolote mitaani kwetu kuhamasisha jinsi ya kujikinga na corona? Kama familia tunahamasishana jinsi ya kutopata hivi virusi hatari? Kama majibu mengi ya maswali haya yanakufikirisha, basi chukua hatua stahiki. Tofauti ya hapo tujiandae kufa sisi na wote katika nyumba zetu kwani ugonjwa huu ni hatari kuliko tunavyouchukulia. Naona tumeachia sana swala hili kwa viongozi wa juu wa kitaifa na vyombo vya habari. Huku ngazi ya chini bado kumepoa SANA kuhusu hatari ya corona. Tuamke na kuchukua hatua.
Post a Comment