YANGA YAMTIMUA KOCHA WAKE LUC EYMAEL KWA UTOVU WA NIDHAMU!
Taarifa rasmi ya Klabu ya Yanga ya kumtimua Kocha wake Mbelgiji ambaye katika tuhuma zake kadhaa dhidi ya Yanga na TFF, alithubutu kuufananisha ushangiliaji wa Wapenzi wa Yanga na nyani au mbwa wanaobweka. Kitendo hiki kimetafsiriwa kuwa ni cha ubaguzi usioweza kuvumiliwa kabisa.
Wakati huohuo Shirika la Soka nchini TFF limetoa tamko la kulaani matamshi ya aliyekuwa Kocha wa Yanga Luc Eymael na kueleza kusikitishwa na matamshi yasiokuwa na maadili na ustaarabu na imeahidi kulifikisha suala hilo katika Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA)ili hatua ya kinidhamu ichukuliwe dhidi yake.
Matamshi ya udhalilishaji ya Luc Eymael aliyarekodi katika mfumo wa Podcast majuzi na kusambaa mitandaoni wakati Yanga ilipotoka sare na timu ya Mtibwa hivyo kuiweka rehani nafasi ya kuwa mshindi wa pili wa VPL. Hata hivyo matokeo ya ushindi 1:0 katika pambano la mwisho kwa Yanga dhidi ya Lipuli jana kuliiwezesha kukamata nafasi hiyo ya pili baada ya washindani wao Azam kutoka suluhu ya 2:2 na Prisons.
Luc Eymael inasemekana hana rekodi nzuri ya kuhitimisha salama mikataba yake ya kazi ya ukocha katika klabu zake za awali alizozifundisha.
Post a Comment